Wejisa Company Limited, ni kampuni ya kizalendo iliyosajiliwa rasmi, inayobobea katika huduma za usimamizi wa taka na usafi wa mazingira. Misingi tunayoizingatia kama kampuni ndiyo nguzo kuu zilizojenga jina la Wejisa kama taasisi ya kuaminika na inayowajibika.
Kupitia kauli mbiu yetu: “Weka Jiji Safi” tumejijengea nafasi kama mshirika wa kweli kuhakikisha miji yetu inabaki salama muda wote. Kipaumbele chetu ni kutoa huduma bora za kuaminika na zinazojali mazingira,huku tukilenga kuwahudumia wateja wetu wote kwa kiwango cha hali ya juu. Kwa pamoja, tunajenga mazingira bora na salama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Discover new jobs in Tanzania (Nafasi za kazi na ajira Mpya), top vacancies, and career opportunities. Visit Mabumbe.tz for employment updates and post job ads.