JINA LA KAMPUNI: DR EAM BIG MICROFINANCE (T) LTD
KUSAJILIWA: Dream Big Microfinance (T) Limited ilisajiliwa mnamo tarehe 8th April, 2018 na msajili wa makampuni na kupata namba ya usajili 125317.
SHUGHULI ZAKE: Dream Big Microfinance (T) Limited inajishughulisha na utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo Tanzania Bara kwa ajili ya kukuza mitaji ya kuendeleza biashara zao. Imepata kibali namba MSP2-0319 kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuendesha biashara ya kutoa mikopo midogo ikifuata sheria ya Microfinance ya mwaka 2018 pamoja na kanuni zake za mwaka 2019.
MAHALI ILIPO: Ofisi za Dream Big Microfinance (T) Limited zipo katika jengo la Condo Investment, ghorofa ya kwanza, chumba namba 110, Kata ya Kaloleni, Manispaa ya Arusha.
NAFASI ZA KAZI: Dream Big Microfinance (T) Limited inatangaza nafasi 15 za kazi ya maafisa mikopo wanawake wenye vigezo vifuatavyo:
ELIMU: Aliyemaliza kidato cha nne mpaka Stashahada (Diploma) kuanzia mwaka 2022 kurudi nyuma.
UMRI: Kuanzia miaka 25 mpaka miaka 35.
MUHIMU: Awe ni mwenyeji anayejua maeneo/mitaa ya Jiji la Arusha na vitongoji vyake.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wote watume maombi kwa barua pepe ya:dreambigmf18@gmailcom au mosielineema@gmail.com.
Waombaji wote watume CV na barua ya maombi tu.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28/02/2025.
Go to our Homepage To Get Relevant Information.
More Information
- Salary Offers Maximum 300,000 per month
- Total Years Experience 0-5