TANGAZO LA KAZI
Kampuni ya Keboguard iliyopo mkoani Arusha inawatangazia nafasi za kazi kwa kada ya Ulinzi kwa mkataba. Hivyo waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma Maombi ya kazi ya nafasi hizo.
- NAFASI: ULINZI (NAFASI 50)
SIFA ZA UJUMLA KWA WAOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na cheti cha mafunzo ya JKT au Mgambo
- Umri kuanzia miaka 18 hadi 40
- Awe na Elimu kuanzia Darasa la saba, kidato cha nne na kuendelea
- Awe hajawahi kushitakiwa kwa makosa yoyote ya jinai
- Awe na akili timamu na afya njema
- Urefu futi 5.6 kwa mwanaume na 5.4 kwa wanawake na kuendelea
- Mwombaji awe tayari kufanya kazi mkoa wowote Tanzania
MWAMBAJI ANATAKIWA KUAMBATANISHA VITU VIFUATAVYO KATIKA BARUA YAKE YA MAOMBI
- Barua ya maombi ya kazi
- Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa ikiwa na picha yake
- Nakala ya kitambilisho cha taifa au mpiga kura
- Barua mbili za wadhamini, picha Pamoja na vitambulisho vyao
- Barua za utambulisho za wadhamini kutoka serikali za mtaa
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuhakikisha kwamba hakuna mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini
- Kuhakikisha kuwa Mali yoyote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake
- Kulinda usalama wa majenga ofisi na mali za ofisi mchana na usiku
- Kuhanikisha milango na madirisha yote inafungwa ipasanyo mwisho wa masaa ya kazi
- Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wanaidhini ya kufanya hivyo
- Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile moto, mafuriko nk na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika .
- Kutoa taarifa namna ya kuboresha huduma za ulinzi mahali pa kazi
- NAFASI: MLINZI WA CONTROL ROOM (NAFASI 3)
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na cheti cha mafunzo ya JKT au Mgambo
- Umri kuanzia miaka 18 hadi 40
- Awe na Elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea
- Awe na uwezo wa kutumia computer
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yanapokelewa kwa njia ya email:hr@keboguard.ac.tz
AU
HUMAN RESOURCE
KEBOGUARD SECURITY CO.LTD
P.O.Box 12523
ARUSHA TANZANIA.
AU
Kuwasilisha ofisini(Hand delivery)
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE: 20/07/2024
Go to our Homepage To Get Relevant Information.
More Information
- Total Years Experience 0-5