MATRONI NA MPISHI WA SHULE

Job Expired

UFALME SCHOOLS

VIKAWE SHULE, KATA YA PANGANI, KIBAHA, PWANI

NAFASI YA KAZI: MATRONI NA MPISHI WA SHULE – UFALME SCHOOLS

Majukumu ya Kazi:

Matroni na Mpishi wa shule ana jukumu la kuhakikisha ustawi, usalama, na afya ya watoto shuleni, hasa wale wanaolala bweni. Majukumu yake ni pamoja na:

Malezi na Ustawi wa Watoto

  • Kuhakikisha watoto wanatunzwa vizuri na wanapata mazingira salama na yenye upendo.
  • Kusimamia usafi wa wanafunzi, mavazi, na nidhamu yao ya jumla.
  • Kusaidia watoto wenye changamoto za kiafya kwa kushirikiana na wahudumu wa afya wa shule.

Usafi na Utaratibu wa Mabweni

  • Kusimamia usafi wa mabweni, vyoo, vitanda, nguo, na vifaa vya watoto.
  • Kuhakikisha watoto wanazingatia muda wa kulala, kuamka, na ratiba ya kila siku.

Uhusiano na Walimu na Wazazi

  • Kushirikiana na walimu kuhakikisha watoto wanapokea malezi bora.
  • Kuwasiliana na wazazi kuhusu maendeleo ya watoto wao, hasa kuhusu afya na tabia zao.

Usalama wa Watoto

  • Kuhakikisha watoto wako salama wakati wote na kuzingatia taratibu za shule.
  • Kuchukua hatua za haraka pale mtoto anapoumwa au kuwa na matatizo yoyote.

Mapishi na Maandalizi ya Chakula

  • Kupika chakula cha shule wakati wa mchana na kuwapikia watoto wa boarding jioni na weekend.
  • Kupika chakula kizuri, chenye lishe, na salama kwa watoto wa umri wa miaka 2 na kuendelea.
  • Kuhakikisha chakula kinaandaliwa kwa wakati na kwa viwango vya juu vya usafi.
  • Kushirikiana na uongozi wa shule kupanga mlo wenye afya kwa watoto.
  • Kuhakikisha chakula kinatosha kwa wanafunzi wote kwa muda wa siku nzima.

 

Usafi wa Jikoni na Vifaa vya Kupikia

  • Kusimamia usafi wa jikoni, vyombo, na sehemu za kula.
  • Kuhakikisha chakula kinatunzwa kwa njia salama ili kuepuka magonjwa ya tumbo.
  • Kuhakikisha kanuni za afya na usafi wa chakula zinazingatiwa.
  • Kuwasiliana na uongozi wa shule kuhusu mahitaji yoyote ya chakula au vifaa vya kupikia.

VIGEZO VYA MUOMBAJI (MATRONI & MPISHI)

Elimu: Awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi, mafunzo ya malezi ya watoto au hotelia/upishi itakuwa kigezo cha nyongeza na faida kwa muombaji.

Uzoefu: Awe na uzoefu wa angalau miaka 2 katika malezi ya watoto na upishi, hasa katika shule au taasisi zinazohudumia watoto wadogo (mwaka 1+).

Sifa za Kibinafsi: Awe msafi, mwenye nidhamu, uaminifu, uvumilivu, na upendo kwa watoto, pamoja na uwezo mzuri wa kuwasiliana na watoto, wazazi, na walimu.

Ustadi wa Kazi: Awe hodari katika kupika chakula, kusimamia usafi wa jikoni na mabweni, na kushughulikia mahitaji ya watoto kwa hekima na busara.

Afya na Uwezo wa Kazi: Awe na afya njema, nguvu za kufanya majukumu mchanganyiko.

 

Jinsi ya Kutuma Maombi:

Tuma Barua ya Maombi ikielezea ujuzi na uzoefu wako. Tuma kwa Email [email protected]  mwisho wa kutuma ni 21/03/2025.

NB: Nafasi hii ni kwa wanawake tuu.

Go to our Homepage To Get Relevant Information.

More Information

  • This job has expired!
Share this job

Contact Us