UFALME SCHOOLS
VIKAWE SHULE, KATA YA PANGANI, KIBAHA, PWANI
NAFASI YA KAZI: MATRONI NA MPISHI WA SHULE – UFALME SCHOOLS
Majukumu ya Kazi:
Matroni na Mpishi wa shule ana jukumu la kuhakikisha ustawi, usalama, na afya ya watoto shuleni, hasa wale wanaolala bweni. Majukumu yake ni pamoja na:
✅ Malezi na Ustawi wa Watoto
- Kuhakikisha watoto wanatunzwa vizuri na wanapata mazingira salama na yenye upendo.
- Kusimamia usafi wa wanafunzi, mavazi, na nidhamu yao ya jumla.
- Kusaidia watoto wenye changamoto za kiafya kwa kushirikiana na wahudumu wa afya wa shule.
✅ Usafi na Utaratibu wa Mabweni
- Kusimamia usafi wa mabweni, vyoo, vitanda, nguo, na vifaa vya watoto.
- Kuhakikisha watoto wanazingatia muda wa kulala, kuamka, na ratiba ya kila siku.
✅ Uhusiano na Walimu na Wazazi
- Kushirikiana na walimu kuhakikisha watoto wanapokea malezi bora.
- Kuwasiliana na wazazi kuhusu maendeleo ya watoto wao, hasa kuhusu afya na tabia zao.
✅ Usalama wa Watoto
- Kuhakikisha watoto wako salama wakati wote na kuzingatia taratibu za shule.
- Kuchukua hatua za haraka pale mtoto anapoumwa au kuwa na matatizo yoyote.
✅ Mapishi na Maandalizi ya Chakula
- Kupika chakula cha shule wakati wa mchana na kuwapikia watoto wa boarding jioni na weekend.
- Kupika chakula kizuri, chenye lishe, na salama kwa watoto wa umri wa miaka 2 na kuendelea.
- Kuhakikisha chakula kinaandaliwa kwa wakati na kwa viwango vya juu vya usafi.
- Kushirikiana na uongozi wa shule kupanga mlo wenye afya kwa watoto.
- Kuhakikisha chakula kinatosha kwa wanafunzi wote kwa muda wa siku nzima.
✅ Usafi wa Jikoni na Vifaa vya Kupikia
- Kusimamia usafi wa jikoni, vyombo, na sehemu za kula.
- Kuhakikisha chakula kinatunzwa kwa njia salama ili kuepuka magonjwa ya tumbo.
- Kuhakikisha kanuni za afya na usafi wa chakula zinazingatiwa.
- Kuwasiliana na uongozi wa shule kuhusu mahitaji yoyote ya chakula au vifaa vya kupikia.
VIGEZO VYA MUOMBAJI (MATRONI & MPISHI)
✔ Elimu: Awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi, mafunzo ya malezi ya watoto au hotelia/upishi itakuwa kigezo cha nyongeza na faida kwa muombaji.
✔ Uzoefu: Awe na uzoefu wa angalau miaka 2 katika malezi ya watoto na upishi, hasa katika shule au taasisi zinazohudumia watoto wadogo (mwaka 1+).
✔ Sifa za Kibinafsi: Awe msafi, mwenye nidhamu, uaminifu, uvumilivu, na upendo kwa watoto, pamoja na uwezo mzuri wa kuwasiliana na watoto, wazazi, na walimu.
✔ Ustadi wa Kazi: Awe hodari katika kupika chakula, kusimamia usafi wa jikoni na mabweni, na kushughulikia mahitaji ya watoto kwa hekima na busara.
✔ Afya na Uwezo wa Kazi: Awe na afya njema, nguvu za kufanya majukumu mchanganyiko.
Jinsi ya Kutuma Maombi:
Tuma Barua ya Maombi ikielezea ujuzi na uzoefu wako. Tuma kwa Email [email protected] mwisho wa kutuma ni 21/03/2025.
NB: Nafasi hii ni kwa wanawake tuu.
Go to our Homepage To Get Relevant Information.
More Information
- Salary Offers Maelewano.
- Total Years Experience 0-5