Email: mabumbe@gmail.com

Mtaalamu wa Kupiga Mbizi (Scubadiver)

Job Expired

Dark Earth Carbon kwa niaba ya Tanganyika Blue (TB), inatafuta Mtaalamu wa Kupiga Mbizi (Scubadiver).

 

Kazi: Mtaalamu wa Kupiga Mbizi (SCUBA Diver)

Mahali: Kigoma

Idara: Ukaguzi wa Vizimba (Cage Inspection)

 

Muhtasari wa Kampuni

Tanganyika Blue inajishughulisha na tasnia ya uvuvi, ikilenga ufugaji wa samaki, usambazaji, na uuzaji wa bidhaa bora za samaki. Tumejikita katika taratibu endelevu za uvuvi na kutoa samaki safi, wenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wetu.

 

Maelezo ya Kazi:

Tunatafuta wafanyakazi wenye uzoefu wa kupiga mbizi kwa kutumia vifaa vya SCUBA kwa ajili ya ukaguzi wa vizimba vya Samaki (fish cages) katika Ziwa Tanganyika. Kazi hii ni muhimu kuhakikisha vizimba (cages) viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa kwa uzalishaji wa samaki wa kibiashara.

 

Majukumu: 

  • Kufanya ukaguzi wa vizimba vya samaki chini ya maji.
  • Kuhakikisha usalama wa vizimba na kutoa taarifa juu ya hali yao.
  • Kusaidia timu ya uzalishaji kwa taarifa zinazohitajika kuhusu vizimba.

 

Sifa zinazohitajika:

  • Uzoefu wa kupiga mbizi kwa kutumia vifaa vya SCUBA.
  • Uelewa wa msingi wa usalama wa kupiga mbizi chini ya maji.
  • Uwezo wa kufanya kazi chini ya maji kwa muda mrefu.
  • Sio lazima kuwa na elimu ya juu, lakini lazima uwe na ujuzi wa kupiga mbizi kwa vitendo.

 

Vigezo vya Ziada: 

  • Cheti cha mafunzo ya SCUBA (itapewa kipaumbele).
  • Afya nzuri na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira magumu.
  • Uzoefu wa awali wa kufanya kazi chini ya maji ni faida na utazingatiwa wa kwanza.

 

Kwa maelezo zaidi na kuomba kazi, tafadhali tuma barua ya maombi na wasifu wako kwa anuani- glory@darkearthcarbon.com, ama Whatsapp +255 738 832 228.

Go to our Homepage To Get Relevant Information.

  • This job has expired!
Share this job

Contact Us

https://mabumbe.tz/wp-content/themes/noo-jobmonster/framework/functions/noo-captcha.php?code=b5f22